Ommy Dimpoz kutumbuiza kwenye tuzo za Afrimma


Ommy Dimpoz atatumbuiza kwenye tuzo za AFRIMMA na zile za African Entertainment Awards mwaka huu nchini Marekani.

Ommy Dimpoz

Ommy ameiambia Bongo5 kuwa hizo ni dalili nzuri kuwa muziki wake unaendelea kufanikiwa zaidi kimataifa.

“Nikijiangalia sasa hivi focus imehamia kimataifa zaidi, hata hivi jana nilikuwa nafanya interview na Sound City, milango inazidi kufunguka zaidi,” amesema. “Hata kwenye tuzo za Afrimma licha ya kupata nafasi ya kuwa nominee, nitakuwa mmoja wa watumbuizaji”
“Pia tuzo zile zingine zinaitwa African Entertainment Awards zinafanyika New York, Marekani tarehe 31 October ambako pia mimi nitakuwa natumbuiza,” ameongeza.
“Kwahiyo mashabiki wangu wajiandae kwa surprise ya kujua kolabo niliyofanya na msanii wa kimataifa, inakuwa video kubwa kutoka kwa director mkubwa, hiyo ndo mipango mipya.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment