Shetta akanusha kufanya biashara ya unga


Hitmaker wa Shikorobo, Shetta amekanusha kuwa hajihusishi na biashara ya madawa ya kulevya kama watu wanavyodai.



Shetta ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM kuwa safari zake anazosafiri ni kwaajili ya biashara ya muziki wake.

“Unajua mtu kinakuumiza kitu labda ukifanya kwa ukweli. Mimi star scandal, I don’t care kwa sababu mimi nafanya maisha yangu, sifanyi biashara hiyo,” alisema.

“Mimi nafanya muziki wangu na muziki unanifanya nifanye biashara nyingine kwa sababu South Africa inasemekena wasanii wengi wanauza madawa ya kulevya kwahiyo nisiende South Africa.”

“Hicho sio kitu cha ukweli, wanasema nakuwa pamoja na watu wanaouza madawa ya kulevya mimi hawajahi kuniambia wanafanya hiyo biashara na sijui kwanini niingiliwe uhuru wa kuwa na marafiki? Labda ningekuwa nawajua ningewapisha ili wasinichafulie jina,” aliongeza.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment