Shilole akaidi adhabu ya Basata!

Msanii Zuwena Mohamed alimaarufu kama Shilole amekaidi adhabu aliyopewa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) iliyomtaka kutoshiriki masuala ya sanaa ndani na nje ya nchi kwa mwaka mzima.

Shilole amekaidi adhabu hiyo baada ya kuonekana akifanya show katika kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimnadi Mgombea nafasi ya urais wa chama hicho Dk. John Magufuli wakati wapo jijini Mbeya siku kadha zilizopita.

Kipindi cha Planet Bongo kilitaka kufahamu endapo adhabu ya msanii huyo imefutwa, na kuwatafuta Baraza la Sanaa Tanzania ndipo hapo Mama Sharua ambaye yupo katika Idara ya kukuza Sanaa na Masoko alipokanusha kufutwa kwa adhabu ya msanii huyo na kusema adhabu yake ipo palepale na kama amefanya shoo amekaidi adhabu hiyo.

"Shilole anatambua wazi kuwa anaadhabu hiyo hivyo kama amefanya shoo sisi kama Basata itabidi tukae chini na kufuatilia juu ya suala hilo na tukigundua kuwa kuna ukweli sheria itachukua mkondo wake," alisema Mama Sharua.

Basata imesema kitendo alichofanya msanii huyo ni wazi kuwa ameshindwa kuheshimu adhabu iliyotolewa na hivyo lazima sheria ichukue mkondo wake kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.

Planet Bongo ilimtafuta msanii Shilole kutaka kufahamu kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo ili hali anatambua kuwa anaadhabu ambayo inamkabili ndipo hapo msanii huyo aliposema kuwa tuyaache hayo mambo kwani ni mambo ya kiserikali zaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment