Siamini kama skendo zinaweza kunisaidia – Country Boy

Rapper Country Boy amedai anaogopa kuwa na skendo kwenye muziki na kwamba mashabiki wake wanamtambua kwa kufanya kazi nzuri peke yake.
COUNTRYBOY1

Akizungumza na Stori 3 ya Planet Bongo kupitia East Africa Radio, rapper huyo alisema haoni kama skendo zina uwezo wa kufanya muziki wake upendwe na mashabiki wake.
“Mimi ni mtu ambaye naamini ninachokifanya,” alisema. Pia nakiamini kile kilichonifanya watu wakanipokea. Mimi siamini kama skendo ndio kitu kinachoweza kunifanya niwe juu kwa sababu sijawahi kuwa na skendo lakini nimepata base kubwa. Watu kufahamu na kupenda kile ninachokifanya ni kwa sababu tu juhudi ya kazi zangu, so inategemea pia skendo zinaweza kukuweka juu lakini mimi siamini kama skendo inaweza niweka juu,” alisema rapper huyo.
“Mimi nafanya kile mashabiki wanataka na kutoa ngoma kali. Mimi nimejaribu tu kuishi bila skendo naogopa skendo. Watu wengine wanaweza wakaichukulia vibaya, mwingine anaweza akakupenda pia kwahiyo mimi naona ni bora mtu asinijue kabisa kuliko anijue kupitia skendo,” alisisitiza Country Boy.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment