Kwa sasa nafanya muziki wa live band zaidi – Grace Matata







Grace Matata ni miongoni mwa wasanii wa kike wa Tanzania wenye uwezo mkubwa wa kuimba.



Licha ya kuwa kwa sasa hasikiki sana, kwa maana kwamba hatoi nyimbo kwa kasi kama wasanii wengine, lakini haimaanishi kuwa ameuweka kando muziki.

Pamoja na mambo mengine anayojishughulisha nayo kwaajili ya kupata kipato cha kuendeshea maisha, Grace ambaye ni mama wa mtoto mmoja amesema kuwa kwa sasa amejikita zaidi na muziki wa live pamoja na kufanya matangazo ya biashara.

Nimeona kukimbizana na media inaleta stress,” amesema Grace Matata alipopiga story na Bongo5. “Sasa hivi nafanya live band zaidi, nertwork yangu kubwa ni events hasa hasa corporate events”.

Ameongeza kuwa bado anaendelea kurekodi nyimbo, lakini amejiwekea utaratibu wa kurekodi na kutoa nyimbo mbili au tatu kwa mwaka.

Toka mwaka huu uanze tayari ameachia wimbo mmoja uitwao ‘Tabibu’ aliomshirikisha Mwasiti, ulitoka mwanzoni mwa June.

Mwaka huu Grace aliyewahi kufanya vizuri na wimbo wake ‘Free Soul’, aliingia kwa mara ya kwanza kwenye tuzo za KTMA 2015 kuwania kipengele cha ‘Mwimbaji Bora wa kike – Bongo Fleva’ ambacho kwa bahati mbaya hakushinda.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment