Stamina adai rappers wengi wanarap tu hawazingatii uandishi



Rapper Stamina amesema rappers wengi wanarap tu bila kuzingatia uandishi bora wa mashairi.



Rapper huyo ameiambia E-News ya EATV kuwa hiyo ni tofauti kubwa kati yake na rappers wengi.

“Tukizungumzia uandishi tunazungumzia kipaji kingine,” alisema. “Ukitaka kujua kama uandishi ni kipaji marapper wangapi wanaraprap tu? Ukisikiliza ngoma yake tangu anaanza mpaka inaisha huelewi nini amekiimba, ameraprap tu. Wenyewe wanaita muziki wa kuswitch. Ukizungumzia muziki wakuswitch, watanzania wangapi wapo vijijini huko hawajui maana ya kuswitch? Je Professor alikuwa anaswitch? Je Solo Thang alikuwa anaswitch? Je Jay Moe alikuwa anaswitch?” amehoji Stamina.

“Japo hata Ulaya wapo kuna watu kazi yao ni kuandika na kuna wengine kazi yao ni kuimba. Lakini ninavyoona mimi Rap conscious ukiwa unaandikiwa mashairi, hiyo ni point of weakness.”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment