Lowassa na Magufuli
Utaratibu wa dunia nzima kwenye midahalo wanahudhuria wagombea na siyo wenye viti wa vyama... Yaani Rais Kikwete aache majukumu yake ikulu halafu aende kwenye vyombo vya habari kufanya midahalo wakati kwenye midahalo wanazungumzia sera za chama husika na sasa aliyebeba sera za CCM ni Ndugu Magufuli.
Baada ya kufanya uchunguzi sababu zifuatazo zimebainika kuwa ndiyo vigezo vya kumfanya mgombea wa UKAWA ndugu Lowassa kususia midahalo hiyo
1. Afya yake ni dhaifu na haimruhusu kukaa muda mrefu bila kupewa dawa ya kumuongezea nguvu. kwenye mikutano yake ya kampeni hajawahi kuzungumza zaidi ya dakika 15, sasa atawezaje kuhudhuria mdahalo akaongea zaidi ya nusu saa?
2. Amehusika sana kwenye kashfa nyingi za ubadhilifu wa mali za umma na hana uwezo wa kukataa ukweli huo, hata alipoulizwa na waandishi wa habari huko Dodoma alikataa kulijibu hilo swali, na endapo atahudhuria kwenye mdahalo wowote hilo swali hawezi kuliepuka
3. Chama chake hakina sera nzuri, anakosa kitu cha kuongea awapo mbele ya watu kwakua chama chake hakijaandaa ilani nzuri yenye sera za kumkomboa Mtanzania. Wakati wenzake wanatoa sera za kupunguza gharama za ujenzi yeye anamwaga sera za kuwatoa jela akina Babu Seya na kubomoa nyumba za nyasi nchi nzima kwa muda wa siku 100
By Aisha Idd
0 comments:
Post a Comment