YAMEBAKI MASAA MANNE (4) DR.SLAA KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI ..KUWEKA HADHARANI KILA KITU






Taarifa nilizozipokea kutoka kwa watu wa karibu kabisa na familia ya Dk Wilbroad Slaa hususani bi. Josephine Mushumbusi ni kwamba Leo saa saba mchana Dr Slaa atatangaza rasmi kujiuzulu ukatibu mkuu wa chadema taifa lakini pia kujivua uanachama wa chama hicho na kutangaza kustaafu siasa.Dr. Slaa atafanya hivyo ikiwa ni hatua yake muhimu ya kusubiri 'muda muafaka' wa kujiunga na chama cha mapinduzi ambacho kimeonesha kumthamini sana kwa wakati huu kuliko chadema.Taarifa zinasema kuwa tangu Dk Slaa aachie ofisi ya katibu mkuu ameonekana kupuuzwa ilihali viongozi wa ccm wa juu wamekuwa wakimjulia hali, kumsalimu na hata kumuomba kumtembelea ingawa amekuwa akiwakatalia na wengine kuishia kufanya mazungumzo na mkewe bi. Josephine Mushumbusi.
"Dr. Amechukizwa sana na dharau za uongozi wa chadema na vijana wao wa mitandaoni kwa kumdharau yeye kwahiyo kesho atatangaza kujitoa katika chama chao na kustaafu siasa ila mwishoni mwa kampeni za Urais kama atahitajika na CCM kuwasaidia kwa makubaliano maalum hatasita kutoa msaada kwao kwani kwake Dr. Magufuli ni rafiki wa karibu kuliko Lowassa wao". Kilieleza chanzo cha karibu na Josephine Mushumbusi.

Tungoje tuone, nini kitajiri leo Serena hotel saa saba kamili mchana
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment