Jose Chameleone: Nasaidia wasanii wachanga kwasababu nilipokuwa msanii mdogo nilinyimwa nafasi hiyo

Jose Chameleone ni mwanamuziki mkubwa wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, lakini ni miongoni mwa wanamuziki ambao hawana ugumu wa kusaidia wasanii mbalimbali hata wadogo pale linapokuja swala la kufanya collabo.

chameleone and Barnaba

Staa huyo kutoka Uganda ameshafanya kazi na wasanii wengi wa Tanzania, wakiwemo wakubwa na wanaochipukia, kitu ambacho amesema anafanya kwa msanii yeyote atakaye hitaji kwasababu yeye binafsi alipokuwa anachipukia alinyimwa nafasi hiyo na wasanii wakubwa.
Chameleone ambaye alitumbuiza jijini Dar wiki iliyopita, na kufanikiwa kushirikishwa na mwanamuziki wa Tanzania Barnaba, ameshare cover ya wimbo huo kwenye ukurasa wake wa Facebook na kutumia nafasi hiyo kuelezea dhamira yake ya kusaidia wasanii.
Ameandika;

“My Entire career is dedicated to giving everybody a chance Musically. This attitude is built on the Fact that as an upcoming Musician I was denied Chance by the established musicians then Until Shanks Vivie Dee Game me a shot that has since then built this Legendary. Brace yourself for another Banger.
LEONE ISLAND MUSIC EMPIRE”



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment