Kocha wa Man United, Louis Van Gaal anaamini Chris Smalling anafaa kuwa nahodha


Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amemtaja mlinzi wa kati wa timu yake, Chris Smalling kuwa baadaye anaweza kuja kuwa nahodha baada ya Rooney na Carrick kumaliza.



Van Gaal ameyasema hayo huku zikiwa zimebakia siku kadhaa tu kuelekea mchezo wa ‘Manchester Derby’ kati ya Manchester United na Manchester City Jumapili hii. Hadi sasa Smalling ndiye mchezaji bora wa klabu tangu kuanza kwa msimu huu.



Van Gaal anaeleza kuwa Smalling ni mchezaji anayeshika maagizo yake haraka. “Uwezo wake wa kujiamini na kuongea ndio siri ya yeye kufanya vizuri” alisema Van Gaal alipoulizwa amemsaidiaje Smalling abadilike haraka ndani ya miezi 12.

Van Gaal anasema, “Rooney ndiye nahodha, na Carrick pia, lakini watakapoondoka, bila shaka Smalling ana sifa zote za kuwa kiongozi hapa”.

Uwezo wa Smalling msimu huu umekuwa ni mzuri siyo Manchester United pekee bali hata timu ya taifa ya England kocha Roy Hodgson anamtazama mlinzi huyo kama sehemu muhimu ya timu ya taifa.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment