Mtayarishaji wa muziki, Man Walter amesema wasanii wakongwe wanashindwa kufanya vizuri kutokana na kushindwa kuendana na mfumo wa muziki wa sasa.
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Man Walter alisema wasanii hao wanahitaji ushauri wa ziada ili wafanye vizuri.
“Unajua muziki umebadilika sana na wengi wanaoathirika na mfumo huu ni wasanii wakongwe, ndio maana wengi wanashindwa kufanya vizuri au kwendana na mfumo huu. Isitoshe muziki wetu kila siku unabadilika, tempo zimeshuka, sasa hivi watu wanapenda muziki wa kusikiliza,” alisema.
“Napata wakati mgumu sana msanii mkongwe akija na kazi yake halafu ukampa ushauri. Kama mimi ni producer ambaye mara kwa mara nakuwa na mtazamo tofauti. Kikubwa nahitaji msanii ama mteja ambaye yupo tayari kushauriwa. Kwahiyo nikikutana na ‘much know’ wale huwa mawazo yangu yanagonga mwamba.”
0 comments:
Post a Comment