Roma ajisalimisha BASATA kuwasikilizisha wimbo mpya aliopanga kuachia kesho siku ya uchaguzi Oct.25

Roma Mkatoliki ameamua kuchukua jukumu la kwenda Baraza La Sanaa Tanzania, BASATA kuwasikilizisha wimbo wake mpya anaotarajia kuuachia Jumapili siku ya uchaguzi Oct.25 ili waupe baraka kuepuka kufungiwa.


roma

Uamuzi huo umekuja kutokana na misukosuko aliyokutana nayo baada ya kutoa wimbo wake wa ‘Viva Roma Viva’ hivi karibuni, ambao BASATA waliufungia kutokana na madai kuwa hakuna ushahidi wa vitu vilivyoimbwa kwenye wimbo huo. .
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Roma alipost ujumbe huu siku ya Jumamosi Oct.24;

“Kesho Ndiyo Ile Tarehe Niliyowaahidi
Kuwa Nitaachia ‪#‎KIBAO‬ Changu Kipya!!!!! /
Na Sasa Naelekea ‪#‎BASATA‬ Kuwasikilizisha Kabisa Kwanza!!! Wakitoa‪#‎GO_A_HEAD‬ Tu Basi Kesho Alfajiri ‪#‎KINANUKA‬ /
WAKIZINGUA NA MIMI NAWAZINGUA!!! /”




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment