Alikiba akanusha tetesi za kumpa ujauzito Jokate
Staa wa Bongo fleva, Alikiba amekanusha taarifa zilizoandikwa na moja ya magazeti ya udaku hivi karibuni, kuwa amempa ujauzito Jokate Mwegelo.
Hivi ndivyo ilivyoandikwa:
“Wakati Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu akihaha kuhakikisha anaitwa mama, habari ‘exclusive’ iliyotua kwenye meza ya gazeti hili inadai kuwa, mwanamitindo anayefanya pia muziki na filamu, Jokate Mwegelo amenasa ujauzito huku muhusika mkuu wa mzigo huo akidaiwa kuwa ni mpenzi wake wa sasa, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mmoja wa watu wa karibu wa Kiba aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema, siku za hivi karibuni Jokate amekuwa na kila dalili za kuwa mjamzito kwani maembe mabichi kwa sana na tumbo limekuwa likimsumbua.
‘Hilo la mimba ndilo linaloonekana kumsumbua kutokana na uumwaji wake na inasemekana ina miezi miwili, so kama mnaweza kufuatilia zaidi, fanyeni hivyo,’ kilidai chanzo hicho.”
Ilisema taarifa hiyo kwenye mtandao wa Global Publishers.
Usiku wa Jumanne (Nov.24) Alikiba na Christian Bella walikuwa wageni kwenye kipindi cha ‘Ala Za Roho’ na mtangazaji Diva The Bawse kupitia Cloudds Fm, na moja ya mambo aliyoyagusia ni pamoja na kuhusu tetesi za kumpa ujauzito Jokate.
“Siwezi kuzungumzia mahusiano yangu- na si kweli natarajia kupata mtoto na Jokate” alikanusha Alikiba.
'Siwezi kuzungumzia mahusiano yangu – na si kweli natarajia kupata mtoto na Jokate' @OfficialAliKiba #AlaZaRoho
Jokate na King Kiba wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara kwa miezi kadhaa sasa, na wamekuwa wakionesha dalili zote kuwa ni wapenzi licha ya kuwa wote wawili hawajawahi kuthibitisha rasmi kuhusu uhusiano wao.
0 comments:
Post a Comment