Album ya Adele ‘25’ kuuza nakala milioni 3 Marekani pekee kwenye wiki ya kwanza
Album mpya ya Adele, 25 inatarajiwa kuuza nakala milioni 3 nchini Marekani katika wiki yake ya kwanza kwa mujibu wa kampuni ya Nielsen Music.
Hadi November 24 album hiyo ilikuwa imeuza kopi milioni 2.8. Miongoni mwa hizo, milioni 1.45 zimeuzwa mtandaoni kwenye iTunes.
25 imeshazidi hadi rekodi ya mauzo ya album kwa wiki mbili tangu kampuni ya Nielsen ilivyoanza kufuatilia mauzo ya album mwaka 1991.
Rekodi ya awali ilishikiliwa na album ya *NSYNC, No Strings Attached iliyouza kopi 2,416,000 katika wiki iliyomalizika March 26, 2000.
Bado wiki haijakamilika tangu album hiyo ya Adele iingie sokoni. Billboard itaripoti mauzo ya wiki nzima ya 25 Jumapili hii baada ya Nielsen kukamilisha kupitia mauzo ya kipindi cha siku saba.
25 iliachiwa Nov. 20 kupitia XL/Columbia Records. Ni album yake ya tatu baada ya 21 na 24.
0 comments:
Post a Comment