Muimbaji wa Kenya, Avril huenda siku za usoni akaonekana kwenye screen yako akiendesha kipindi cha TV.
Avril ameiambia Word Is ya gazeti la The Star la Kenya kuwa amekuwa akifuatwa na watu wengi wanaompa ofa ya kufanya talk show lakini bado hajazitilia maanani.
Yeye mwenyewe pia amesema kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa kuendesha kipindi cha TV na kuna uwezekano wa kufanya hivyo siku za usoni.
“Ingawa muziki ni kitu ninachokipenda zaidi, nimewahi kupenda televisheni pia. Labda siku za usoni ninaweza kujikuta nikiwa muongozaji wa talk show. Nimekuwa nikipewa ofa nyingi lakini najiskia kuwa karibu na muziki wangu zaidi na ninaupa muda unaohitaji kwa sasa,” alisema.
“Lakini naendelea kuwa na matumani kuwa siku moja nitakuwa na talk show yangu kwenye TV.. Labda cha mapishi au kitu kingine,” aliongeza.
Hivi karibuni Avril aliachia video ya wimbo wake No Stress aliomshirikisha AY. Itazame hapo chini.
0 comments:
Post a Comment