Chagga Barbie ndiye ameziba nafasi ya Shamsa Ford kwa Nay Wa Mitego? Nay azungumza


Jimbo la mapenzi la Nay Wa Mitego liko wazi toka aachane na aliyekuwa cousin mpenzi wake Shamsa Ford, lakini swali ni kwamba ni mrembo gani aliyerithi nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Shamsa ambayo huenda kuna warembo wengi wanaitamani?
Chagga na Nay

Kama unamfatilia Nay Wa Mitego kwenye akunti yake ya Instagram sina shaka utakuwa umeanza kuona dalili za kuwa kuna mpenzi mpya ‘mteule’ anayesubiri ‘kuapishwa’ na kuwa rasmi.
Chagga Barbie sio jina geni, ndio yule aliyezitawala headlines nyingi alipokuwa mpenzi wa Prezzo, jina lake halisi ni Starlisha Tillya lakini sasa anatumia jina la Chagga Empress Instagram.



chagga2

Nay na Chagga ambaye ni Mtanzania aishiye Marekani wamekuwa wakiweka post zinazoashiria kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao zaidi ya urafiki wa kawaida, lakini Nay amesisitiza kuwa hawajaingia kwenye ukurasa wa mahaba japo Nay amekiri kuwa anampenda sana Chagga Barbie.
Novemba 11, Chagga alipost video akisema anampenda Nay, na Nay aliirepost na kuandika “Love you too bby Mtag umpendae @chaggaempress @chaggaempress”.



Nay a.k.a True Boy amefunguka kuhusu yeye na Chagga,
“Naomba tu watu wajue ni mwanamke ambaye ninampenda, nampenda the way alivyo ni mwanamke mzuri anavutia sio vinginevyo, labda ikija ikatokea akiwa mwanamke wangu itakuwa ni poa zaidi lakini for this time nampenda the way alivyo” Nay ameiambia Bongo5.

chagga-1
Aliendelea,

“Mimi na Shamsa tulishaachana muda mrefu tumebaki washkaji ana bwana yake nafikiri watu wanaona kwenye page yake anampost, lakini mwisho wa siku nafasi ikishaachwa na mtu watu watajua wataona tu dalili, for this time sidhani kama natakiwa kuongea mengi sana nafikiri watu wataona, lakini watu wajue kwamba Chagga ni mwakamke ambaye nampenda namkubali amekuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ni mwanamke mzuri so haijafikia hatua ya kuwa na mahusiano ya kihivyo ila ikifikia watu wataona coz tuko karibu.” Alisema Nay.
Nay amesema kuwa yeye na Charga Empress bado hawajakutana lakini watakutana hivi karibuni.
“Nafikiri tutakutana hivi karibuni, hivi karibuni tutakuwa pamoja bado hatujaonana”.- Nay


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment