Baada ya kurudiana Kylie Jenner athibitisha kuwa ndoa yake na Tyga inakuja
Baada ya kudaiwa kuachana siku chache zilizopita, rapper Tyga na mrembo kutoka kwenye familia maarufu ya The Kardashians, Kylie Jenner walionekana pamoja baada ya tuzo za ‘American Music Awards’ Jumapili iliyopita, ikiashiria kuwa wamemaliza matatizo waliyokuwa nayo.
Tyga aliyekuwa amevaa suti ya blue pamoja na Kylie aliyekuwa amevaa kivazi cheupe walionekana wakiwa wameshikana mikono baada ya tuzo hizo.
Wakati wakipanda gari ili kuelekea kwenye after party ya Justin Bieber, paparazzi mmoja alimuuliza Kylie kama yeye na Tyga watafunga ndoa, na jibu lake lilikuwa ‘YES’ huku akiingia kwenye gari ba boyfriend wake.
0 comments:
Post a Comment