Fella aeleza kwanini amemshauri Berry Black kuhamia Dar


Meneja wa Mkubwa na Wanae, TMK Wanaume Family pamoja na Yamoto Band, Mkubwa Fella amesema amemshawishi msanii wake mpya Berry Black kutoka Zanzibar na kuhamia Dar es salaam ili kuwa karibu na vyombo vya bahari.



Mkubwa Fella, ameiambia Bongo5 kuwa uwamuzi wa Berry Black kuishi Dar, kutamsaidia msanii huyo kusambaza kazi zake vizuri kwa kuwa yupo karibu na vituo vya habari.

“Muziki ni popote lakini tatizo ni usambazaji, ndo maana tukaamua ahamie hapa Dar ili tuweze kusambaza kazi zake hata kwa miezi mitatu kwanza, tuzunguke kwenye media kwa ajili ya interview na baada ya hapo anaweza kurudi Zanzibar, lakini wakati tayari nyimbo zake zipo sehemu mzuri,” alisema Fella.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment