Si vijana tu wanaopagawa na ngoma mpya ya Joh Makini aliyomshirikisha AKA, ‘Don’t Bother.
Mama yake mzazi na Dully Sykes naye ni shabiki wa ngoma hiyo.
Akizungumza XXL ya Clouds FM, Dully alisema mama yake mara kwa mara amekuwa akijaribu kuuimba wimbo huo unaofanya vizuri kwa sasa.
“Mama yangu anapenda sana hip hop na sasa hivi anapenda sana na ananiimbiaga Don’t Bother,”alisema Dully.
“Don’t Brother ndio nyimbo yake ya Joh Makini. Mama yangu ni shabiki wa Hip hop, ni shabiki mkubwa wa Fid Q pamoja na Joh Makini, Mwana FA. Pia anapenda kwa sababu anapenda mashairi.”
0 comments:
Post a Comment