Joh Makini ana ujumbe kwa wasanii waliokata tamaa
Hitmaker wa Don’t Bother, Joh Makini amewataka wasanii kutokata tamaa hata wakiwa wametoa ngoma nyingi bila mafanikio.
Akizungumza na Stori Tatu kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Joh alisema wapo waliotoa ngoma 30 bila mafanikio lakini wimbo mmoja tu ukaja kuwabadilishia maisha yao.
“Kuna watu wanaimba nyimbo 10,20 hadi 30 lakini bado wanakuwa na maisha mabovu lakini anakuja kutoa wimbo wa 40 unabadili maisha yake yote,” alisema. “Lakini hata wimbo mmoja ukiutilia nguvu ukamwomba Mungu ukatanguliza juhudi zako zote unaweza kufanikiwa. Lakini muziki kama ni maisha yako ni maisha kama maisha ya watu wengine ni kazi kama kazi nyingine kwamba kuna wakati mgumu, kuna mitihani, kuna wakati unatakiwa kuwa mvumilivu,” alisisitiza.
“Unatakiwa usikate tamaa, ujifunze kila siku unapolose kimoja unaweza ukapoteza thamani ya unakoelekea. Kwahiyo vitu vyote hivyo ni package, unatakiwa uhakikishe unavifanya, unarekodi sana, tafuta idea, unajifunza vitu vingi, unasikiliza muziki wa watu wengine hivyo tu.”
0 comments:
Post a Comment