Ex wa Nicki Minaj kwenda kortini, ni kudai kulipwa kwa kushiriki kuandaa album tatu za rapper huyo
Aliyekuwa boyfriend wa Nicki Minaj, Safaree Samuels anaenda mahakamani kushtaki kudai haki yake.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Samuels anataka alipwe mpunga wake kwa kuchangia kutengenezwa kwa album tatu za Nicki, The Pinkprint, Pink Friday, na Pink Friday: Roman Reloaded.
Pia anataka alipwe kwa kuhusika kwenye singles kubwa zikiwemo “Only” ambayo ex wake amewashirikisha Chris Brown, Drake, na Lil Wayne, “Flawless (Remix)” akiwa na BeyoncĂ©, na “Feeling Myself.”
Samuels ambaye pia ni rapper amesema alikuwa na mchango mkubwa katika kutengeneza muziki wa Nicki. Nicki alimtambua kama executive producer kwenye album za Pink Friday and Pink Friday: Roman Reloaded.
Safaree anatarajia kuonesha ushahidi wa video zinazowaonesha akifanya kazi na Nicki, sauti na video kutoka kwenye recording sessions. Pia ana mashahidi lukuki wa kuthibitisha madai yake. Tayari ameshaajiri wakili na muda si mrefu kesi inaanza.
Wawili hao waliachana mwaka jana baada ya kuwa pamoja kwa miaka 12.
0 comments:
Post a Comment