Nikki Wa Pili asema hapendi michoro ya tattoo kwa sababu ni fasheni itakayopotea


Rapper wa kundi la Weusi, Nickson Simon maarufu kama Nikki Wa Pili amesema michoro ya tattoo wanayojichora watu wengi maarufu ni fasheni, hivyo ipo siku itapita na kuonekana haina maana tena, ndiyo maana yeye haipendi.



Akizungumza na MTANZANIA, Nikki alisema kuwa sifa moja ya fasheni ni kuvuma na kupotea, hivyo ana hofu ya kuchora tattoo kwa kuwa itafika kipindi michoro hiyo itakuwa siyo ujanja tena.

“Ile ni fasheni, watu wanachora na wanapendeza, lakini hawajui kuwa sifa kubwa ya fasheni ni kuvuma na baada ya muda hupotea ili kupisha fasheni mpya, sasa itakuwa vipi kama ulijichora mwili mzima halafu baadaye tattoo ikawa si ishu,” alisema Nikki.

Rapper huyo ambaye ameachia single mpya ‘Baba Swalehe’ siku si nyingi, ameongeza kuwa anategemea kuachia video ya wimbo huo hivi karibuni.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment