Tyson Fury amchapa Klitschko na kutwaa ubingwa wa WBA, IBF na WBO
Bondia kutoka Uingereza, Tyson Fury ameshinda moja ya pambano kubwa katika historia ya maisha yake kwa kumpiga Wladimir Klitschko na kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani.
Fury, aliibuka mshindi wa jumla ya pointi baada ya marefarii wote watatu kumpa pointi nyingi zaidi ya Klitschko.
Muingereza huyo alizoa alama 115-112, 115-112, 116-111 na hivyo kutawazwa bingwa wa dunia wa uzani wa juu wa taji la WBA, IBF na WBO
Tyson Fury mwenye miaka 27 amekuwa miongoni mwa waingereza walioingia katika orodha ya mabingwa wa dunia wa uzani wa juu wa ndondi baada ya Bob Fitzsimmons, Lennox Lewis, Frank Bruno na David Haye.
0 comments:
Post a Comment