Andy Murray awa bingwa wa Davis Cup
Mcheza tennis bora kutoka Uingereza, Andy Murray amechukua ubingwa wa michuano ya Davis Cup ya mchezaji mmoja mmoja.
Timu ya Uingereza imetwaa taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1936 baada ya Murray kumshinda Mbelgiji David Goffin
Murray alimshinda mpinzani wake kwa jumla ya seti 6-3 7-5 6-3 na kumfanya Goffin kupoteza kwa jumla ya 3-1. Nyota huyo amejiongezea historia nzuri baada ya kuwa ametwaa mataji ya michuano ya Wimbledon, michuano ya wazi ya US Open na ile ya michezo ya Olimpiki.
0 comments:
Post a Comment