Rapa Mabeste ameweka wazi jinsi msanii mkongwe kwenye muziki Dully Sykes alivyomsaidia katika wakati mgumu maishani mwake.
Mabeste ambaye yupo katika mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka katika mbuga za Manyara National Park Arusha, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa Dully ndiye Godfather kweye muziki wake.
Rapa huyo alisema kipindi chote alipokuwa anahangaika kuhusu muziki, Dully Sykes ndiye alikuwa msaada kwake, kuanzia kuvaa, kula na kulala na aliishi nyumbani kwa Dully kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Mabeste amekanusha taarifa zinazozagaa kuwa amepotea baada ya kuachana na label ya B’Hits.
“Niliondoka B’Hits nikiwa nimepanga chumba kimoja hata TV sina, lakini nilipoanza kufanya kazi zangu mwenyewe nikahama Mbagala nikahamia Kinondoni nikapanga upande mzima wa nyumba, nikanunua gari na maisha yakaendelea kama kawaida, kwahiyo kimuziki nilishuka lakini sikuyumba kimaisha,” alisema Mabeste.

0 comments:
Post a Comment