Meek Mill kukosa shavu la kuigiza filamu ya Will Smith kutokana na kesi yake


Rapper Meek Mill atashindwa kuigiza uhusika wake katika filamu ya Will Smith kutokana na hivi karibuni kupatikana na hatia ya kukiuka masharti ya muda wa matazamio aliopewa na mahakama kufuatia kesi ya miaka 15 iliyopita ya kumiliki silaha na madawa ya kulevya.




Rapper huyo wa Philadelphia, anatarajiwa kusomewa hukumu yake February 5.

Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six, Meek Mill alikuwa amepanga kusafiri kwenda Hollywood November kujadili uwezekano wa kuigiza kwenye filamu iitwayo ’12 O’Clock Boys’ inayotayarishwa na kampuni ya Will Smith, Overbrook Entertainment lakini alishindwa kwakuwa alitakiwa kuchukua vipimo vya mkojo katika kipindi hicho.

Meek Mill alikuwa aigize kama Wheelie Wayne kwenye filamu hiyo inayozungumzia maisha ya waendesha piki piki kwa fujo katika mji wa West Baltimore.

Pamoja na hivyo, Meek Mill atalazimika pia kukosa show na mpenzi wa Nicki Minaj huko Las Vegas ambako angelipwa $140,000 kwa show hiyo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment