Mourinho anaweza kwenda wapi?






Mourinho amefutwa kazi na Chelsea baada ya klabu hiyo kutofanya vyema msimu huu

Baada ya kufutwa na Jose Mourinho kufutwa kazi Chelsea jana, miezi saba tu baada yake kupeleka taji la Ligi ya Premia Stamford Bridge, wengi wanauliza ataelekea wapi.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amefanikiwa sana na, kando na Chelsea, amekufunza katika klabu kubwa Ulaya kama vile Porto, Inter Milan na Real Madrid.

'The Special One', kama alivyojiita, ametimuliwa Chelsea klabu hiyo ikiwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja.

Ataelekea wapi sasa? Hizi hapa ni baadhi ya klabu ambazo watu wanatarajia huenda akaenda.

Manchester United

Mourinho alipigiwa upatu kumrithi Sir Alex Ferguson alipostaafu 2013 na amekuwa akisifu sana klabu hiyo ya Old Trafford.


Uhusiano kati ya Van Gaal na mashabiki wa Man Utd umedorora

Kocha wa sasa Louis van Gaal anaonekana kutatizika na hajaweza kuwafurahisha vyema mashabiki.

Real Madrid

Hasimu wake wa muda mrefu Rafael Benitez, ndiye mwenye usukani kwa sasa Bernabeu lakini amekosolewa sana. Majuzi, Madrid walichapwa 4-0 El Clasico mikononi mwa Barcelona.

Rais wa sasa wa Real Madrid Florentino Perez ni shabiki mkubwa wa Mourinho.

Mourinho aliondoka Real 2013 baada ya mambo kuharibika, lakini je anaweza kwenda kumalizika kazi ambayo huenda anahisi hakuweza kuimaliza?

Bayern Munich

Mourinho ameshinda mataji Ligi ya Premia, La Liga na Serie A lakini wasifu kazi wake hauna Bundesliga popote, na ni klabu moja pekee ambayo inaweza kumtimizia hilo.

Bayern Munich karibuni huenda wakalazimika kutafuta mtu wa kujaza nafasi ya Pep Guardiola ambaye anakamilisha mkataba wake Juni mwaka ujao.


Ancelotti aliondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu

Watahitaji kocha wa haiba kubwa. Mtu pekee ambaye huenda akampa ushinda Mourinho ni Carlo Ancelotti.

Kukosa Kazi

Sifa za Mourinho na kukorofishana na watu huenda zikamfanya kutopendwa na klabu nyingi. Lakini upande mwingine klabu zitaangalia tajriba yake na uwezo wake wa kushinda vikombe. Kwa hivyo, itakuwa vigumu sana kwake kukosa kazi. Labda mwenywe aamue kutochukua kazi yoyote kwa muda kama alivyofanya Pep Guardiola.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment