Q-Chief apewa darasa na Master J kuhusu muziki wake



Q-Chief amesema hivi karibuni alikutana na mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Master J aliyemkalisha kitako kumpa darasa kuhusu muziki wake.


Muimbaji huyo aliyeachia wimbo ‘Mkungu wa Ndizi’ akiwa na TID hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa ujumbe aliopewa na Master J umemfanya aongeze mapambano zaidi.

“Nimekutana na Master J, na alichoniambia nisimame pale ambako nakusudia kusimama kwa sababu mimi nimepigana sana kurudi hapa nilipo sasa na mashabiki wamepokea Mkungu wa Ndizi na kuufanya wimbo mkubwa sana na hauwezi kufa leo au kesho,” alisema Q-Chief.

Aliangoza, “Pia kwenye video kaniambia nifanye kitu kikubwa zaidi. Kwahiyo amenipa michongo na akina Justin Campos pamoja na Godfather akanishauri nionane na Justin Campos nikaongea naye kwenye simu. Khahiyo kila kitu kinaenda sawa, watu na mashabiki wangu wasubirie kazi nzuri.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment