Sikuwahi kuagiza mtu asameweke kodi, msinilamu, mwacheni Magufuli awanyooshe – Kikwete
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amelazimia kutumia mtandao wa Twitter kujibu tuhuma zinazosambaa kuwa katika uongozi wake aliagiza kusamehewa kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara.
London, 11th July 2012. London Summit on Family Planning
Hiki ndicho alichoakiandika:
Wako watu katika vyombo vya habari na mitandao wanajaribu kunihusisha na ukwepaji wa kodi. Nataka kuwaambia, wanapoteza wakati wao bure.
Tumeongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 177 mpaka shilingi bilioni 900 wakati ninaondoka madarakani.
Kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 177 hadi 900 ni matokeo ya kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na kubana ukwepaji.
Watu wenye tabia ya kukwepa kodi hawaachi, huendelea wakati wote na ndio maana mapambano dhidi yao lazima yaendelee wakati wote.
Lazima tumuunge mkono Mheshimiwa Rais kuendeleza mapambano dhidi ya wakwepa kodi kwani ni mapambano endelevu na ya lazima.
Sijawahi wakati wangu, kuagiza mtu yeyote asamehewe kontena lisilipiwe kodi. Ningefanya biashara hiyo tusingefika bilioni 900 toka 177.
Wamekaa wanasumbuka, wasinilaumu mimi, Magufuli ameshawashinda. Mgombea mzuri, wananchi wamemkubali, amekuwa Rais wao, anawatumikia.
Wenye uongo huu wanishambulie mimi, Rais aendelee kufanya kazi zake. Kunishambulia pia ni kupoteza muda, kwa sababu mimi sigombei tena.
Niliyekuwa Rais sikuagiza, sidhani kama mke wangu au mwanangu Ridhiwani anaweza kufanya hayo, akasikilizwa; ni siasa za walioshindwa.
Nataka kuwahakikishia kuwa sikuwahi kutoa agizo kwa mtu yeyote anayestahili kulipa kodi, asilipe kodi, wanaosema hayo wanapoteza muda.
0 comments:
Post a Comment