Eto’o avuliwa majukumu ya ukocha



Eto'o alifanywa mkufunzi wa muda Desemba

Nahodha wa zamani wa Cameroon Eto'o amepokonywa majukumu yake kama kaimu kocha mchezaji katika klabu ya Antalyaspor ya Uturuki.


Nafasi yake imechukuliwa na Jose Morais, ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Chelsea, chini ya Mreno mwenzake Jose Mourinho hadi Desemba.

Morais, ambaye alihusishwa na kuhamia Swansea, pia alikuwa na Mourinho Real Madrid na Inter Milan.

Eto'o alichukua majukumu ya ukufunzi mapema Desemba na alishinda mechi zake mbili za kwanza kabla ya kushindwa mechi mbili na kutoka sare mechi moja.

Morais, 50, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja unusu kwenye sherehe iliyoongozwa na mwenyekiti wa Antalyaspor Gultekin Gencer, klabu hiyo imesema kupitia taarifa.

Eto’o, mchezaji wa zamani wa Barcelona na Chelsea, ataendelea kukaa katika klabu hiyo ya Uturuki kama mchezaji.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment