Mshambuliaji wa Leicester Vardy kufanyiwa upasuaji



Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy atakuwa nnje ya wa uwanja kwa wiki mbili baada ya kufanyiwa upasuaji.



Mchezaji huyo wa timu ya taifa Uingereza amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye mtoki wake, kituo cha redio cha BBC cha Leicester kimeripoti.

Vardy amekuwa na msimu mzuri sana hadi saivi ana mabao 15 aliyoyafunga Ligi ya Premia yamesaidia Bweha hao kupanda hadi nambari mbili ligini.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 amechezea klabu hiyo mechi 24 msimu huu.

Vardy alicheza kwenye kikosi cha mkufunzi Roy Hodgson cha Uingereza kilichofuzu kwa michuano ya Euro 2016.

Alichezea klabu yake dakika zote 95 mechi dhidi ya Bournemouth ambayo walitoka sare ya 0-0 Jumamosi.

Source: BBC

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment