Mwana FA adai kucheza ndondi kumemsaidia kupunguza hasira



Mwana FA amesema mara nyingi akivurugwa na mtu, hasira zake huzimalizia katika mazoezi yake ya ndondi.



Rapa huyo ambaye amedai yupo kwenye mchezo huo kwa miaka mitatu mpaka sasa, alikiambia kipindi cha 360 cha Clouds TV kuwa wakati anaanza mchezo huo alikua ni mtu wa hasira lakini kadri alivyoendelea kuucheza zimepotea.

“Boxing inanisaidia sana,” alisema. “Nikiwa na hasira na mtu naenda zangu kwenye punching bag nalitandikaa mpaka basi. Nina miaka kama mitatu, minne nafanya boxing, baada ya kuanza kufanya boxing hata hasira zangu zimepungua kabisa, pengine labda ni nidhamu ambayo inakuja baada ya kucheza huo mchezo,” alifafanua FA.

Katika kipindi cha miaka hiyo mitatu hata muonekano wa rapper huo umebadilika na kuwa mtu aliyejaza zaidi ukilinganisha na awali alivyokuwa mwembamba.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment