Rais Wa Marekani, Barack Obama Amwaga Machozi Hadharani




Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa Risasi nchini humo.


Obama aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatete ni kwa manufaa yao wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na wala hana mpango wa kugombea.

Rais Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwapekua na kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha.Kwa sasa, takwa hilo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa.

Wauza silaha ambao hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wateja wao iwapo wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili.

Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.

==>Tazama Video Hii 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment