Saudia na Iran zaombwa kuondoa uhasama





Rais wa Iran Hassan Rouhani na kiongozi kutoka Saudi Arabia

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameomba mataifa ya Saudi Arabia na Iran kumaliza mozozo wa sasa wa kidiplomasia kati yao.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje amesema kwamba Bwana Kerry amewasiliana kwa njiya ya simu na Mawaziri wa mambo ya nje kutoka pande mbili. Saudi Arabia ilikatiza uhusiano wa kidiplomasia na Iran baada ya waandamanaji kushambulia ubalozi wa Saudia mjini Tehran.


Kumekua na maandamano kulaani kunyongwa kwa kiongozi wa Kiongozi wa Kishia Nimr Al-Nimr

Kumekuwa na misururu ya maandamano kulaani kunyongwa kwa kiongozi wa madhehebu ya Kishia nchini Saudia.

Iran inayofuata madhehebu ya Kishia na Saudi Arabia inayofuata madhehebu ya Kisunni zimekua zikikabiliana katika vita vinavyokumba mataifa ya Yemen na Syria.

Baraza la Usalama limekosoa vikali kulengwa kwa ubalozi wa Saudia huko Tehran lakini taarifa hiyo haikugusia kunyongwa na kiongozi wa kishia Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine waliopatikana na hatia ya ugaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment