‘Haters’ huwezi bishana nao – Ali Kiba



Staa wa muziki Ali Kiba amesema Adam Juma aliongea ukweli ndio maana ‘haters’ wakamtukana.


Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Ali Kiba alisema watu hao wanaopinga ukweli wana nia ya kumrudisha nyuma kwa kumvunja moyo.

“Nimesikia hiyo ya Adam, Adam namweshimu sana. Adam ni legendary kwa hizi video za muziki kwa hapa Tanzania, yeye ndiye aliyeutoa muziki wa Tanzania na akaupeleka katika ngazi kubwa sana,” alisema Ali Kiba.

“Jinsi sisi tunavyo improve na yeye anaimprove vilevile. Kwa sababu alikotoka ni tofauti na aliko sasa hivi, vilevile Adam anasoma na kujifunza vitu vipya. Aliongea vitu vya kitaalumu mule ndani, lakini kuna watu ambao wao always wanakuwaga ni ‘haters’ na hater huwezi bishana nae. Kwahiyo wana hater hata wanajua au hawajui na wana crash ilimradi kumrudisha mtu nyuma. Kwa sababu Adam aliongea kiufundi na unapokuwa umeongea kiufundi inakuwa inawauma watu. Kwahiyo hii hali lazima uielewe, mimi mwenyewe natukanwa sana, inaweza ikawa kwenye good way or bad way, lakini sitakiwi kufocus of that,”aliongeza.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment