Msanii wa muziki wa Hip Hop Bill Nas amefunguka kwa kusema kuwa wimbo wake ‘Raha’ aliyomshirikisha rapa Nazizi wa nchini Kenya ndio wimbo wake mkubwa kuliko Ligi Ndogo.
Rapa huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo Ligi Ndogo, ameiambia Bongo5 kuwa wimbo wa Raha ulimfikisha mbali zaidi kimuziki kuliko Ligi Ndogo.
“Unajua tatizo lipo hivi, Raha ni wimbo ambao umetoka muda kidogo kabla ya Ligi Ndogo ni kama mwaka mmoja hivi. Lakini jinsi nilivyoimba kwenye Raha na Ligi Ndogo ni tofauti, pia Raha ilitoka na video na Ligi Ndogo haikutoka na video. Lakini Raha ndio wimbo ambao umenitambilisha zaidi na mkubwa hata kwenye show zangu Ligi Ndogo inafanya vizuri lakini Raha inafanya vizuri zaidi hususan mikoani,” alisema Bill Nas.
0 comments:
Post a Comment