King Dodoo ambaye ni meneja wa msanii Christian Bella amezungumizia ngoma mpya ya Christian Bella na kundi la Weusi, na kwa nini Weusi? Mahadhi ya wimbo na maana yake, pia unatoka lini?
Akiongea na mtangazaji Smashratino wa Radio Rasi Fm ya DODOMA, King Dodoo alisema:
Naongea kama meneja wa Bella kutoka na wimbo mpya wa Bella na Weusi. Unajua muziki ni kufurahisha watu na ndia maana Bella ameamua kufanya kazi na Weusi na kuwafanya mashabiki pia wa Hip Hop wapate ladha tofauti nakuonyesha kuwa Bella anaweza kumix Dance na Hip hop na pia anaweza kufanya kazi na kila msanii. Nafikiri wiki ijayo wimbo utakuwa tAyali na wimbo unaitwa “Utatunza Penzi Langu.”
“Maana halisi ya wimbo ni kwamba watu wengi sana wanapenda kuiga katika mapenzi badala ya mtu kukaa na mpenzi wake akatulia unakuta wanaiga maisha ya katika mitandao maana maisha ya mtandao kila mtu anaishi maisha ya kishua nafikiri hiyo ndo ladha ya huo wimbo,” aliongeza.
0 comments:
Post a Comment