Mchezaji nyota wa Barcelona, Neymar, ambaye anatuhumiwa kwukwepa kulipa kodi na Mahakama moja ya Brazil imezuia mali za nyota huyo.
Mahakama hiyo ambayo ipo Sao Paulo ilitangaza kuwa inatoa waranti ya kuzuia mali yenye thamani ya takriban dola milioni 50 ya mchezaji huyo wa Brazil.
Mali hizo ambazo ni ndege,jahazi la kifahari na Mali nyengine.
Neymar mwenye miaka 23 ametuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2011 na 2013 na anakabiliwa na mashataka ya kujibu.
Hata ivyo nyota huyo amekana kufanya makosa yoyote.
Miongoni mwa mali zingine zilizozuiwa ni kampuni tatu zinazomilikiwa na familia yake.
Waendesha mashtaka wanamtuhumu Neymar kwa kuanzisha kampuni ambazo zilimsaidia kulipa kiwango kidogo cha ushuru.
Wanataka alipe dola milioni 16 kama kodi ambayo haikutangazwa.
Mahakam hiyo iliagiza mali yake kuzuuliwa ili kuhakikisha kuwa anafanya malipo hayo pamoja na faini.
Neymar anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama na kwamba sio rahisi kwa yeye kuhudumia kifungo,kulingana na mkaguzi mmoja wa maswala ya fedha.
0 comments:
Post a Comment