Moja ya ngoma ambayo inatikisa kwa sasa mtaani, kwenye promotion na club ni ngoma ya Kamatia yake Aika naNahreel wanao unda kundi la Navy Kenzo. Video ya ngoma hiyo imekita kila kona kutokana na ubora wake warembo waliopo kwenye ngoma hiyo.
Kati ya mastaa wakike ambao wapo kwenye list ya uvaaji wa kiheshima huwezi kumsahau Aika, Lakini kwenye video hii anaonekana akiwa kavaa kibukta kivupi kinacho muacha mapaja wazi.
Ndni ya Friday Night Live show inayo rushwa na EATV kwaujumla Navy Kenzo walijibu kuhusiana na suala hilo.Nahreel akiwa mpenzi wa Aika alisema yeye binafsi alimshawishi sana Aika hadi kukubali kuvaa nguo hiyo kwakuwa ilikuwa ni agizo la director ili video iweze kuvutia.
Lakini kwenye mahojiano na mtangazaji wa show hiyo Sammisago aliuliza kuhusiana na mafanikio ya wanamuziki hwa ambapo Nahreel alisema kwasasa ameshiriki kuandaa ngoma itakayo kuwepo kwenye album ya mwanamuziki Patoranking "Kuna album ya Patoranking ninahusika, Patoranking nimempatia nyimbo mbili ambazo zilikuwa zetu kabisa" alisema Nahreel.

0 comments:
Post a Comment