Romelu Lukaku: Mshambuliaji bora kwangu ni Robin van Persie



Mshambuliaji wa klabu ya Everton Romelu Lukaku anaamini kwamba mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal,Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi Robin van Persie ndiye mshambuliaji mwenye ‘movement’ ambaye amewahi kumshuhudia.



Mholanzi huyo amabye aliitumikia Arsenal kwa misimu nane na kuibuka mfungaji bora katika msimu wake wa mwisho akiwa na klabu hiyo kabla ya kuhamia Manchester United na kushinda ubingwa wa ligi ya England.

Lukaku, ambaye hadi saivi amefunga magoli 16 msimu huu, aliulizwa aseme mshambuliaji ambaye amewahi kumvutia wakati akichipukia katika soka la kimataifa, na ndipo alipomtaja Robin Van Persie.



“Kwa wakati fulani nilikuwa nampenda sana Robert Lewandowski wakati alipokuwa akianza kucheza Dortmund. Nilikuwa pia nikimtazama sana Zlatan Ibrahimovic. Adriano, kwenye ubora wake akiwa Inter Milan, alikuwa hatari sana,” Lukaku alisema.

“Van Persie alikuwa na movement za hatari sana. Alipokuwa Arsenal na kushinda kiatu cha dhahabu, nilishuhudia movement za hatari sana kutoka kwake.

“Hata katika msimu wake wa kwanza akiwa Manchester United, walishida ubingwa kwa sababu alifunga takriban magoli yote yaliyopelekea kutwaa ubingwa.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment