BASATA hawajaufungia wimbo wangu – Nay wa Mitego
Rapper Nay wa Mitego amekanusha taarifa zilizoenea kuwa, baraza la sanaa la taifa, BASATA limeufungia wimbo wake wenye utata, Shika Adabu Yako.
Nay ametoa ufafanuzi huo kwenye Instagram kwa kuandika:
Pale unaposikia eti kuna wasiopenda kuambiwa Ukweli wamezusha Eti Wimbo wa #ShikaAdabuYako Basata wamefungia. Guys Wimbo haujafungiwa na Basata awajafungia Wimbo ila wale wenye Team zao kwenye mitandao wamechanwa kwenye #ShikaAdabuYako ndio wameufungia kwenye Masikio Yao sababu ya hawataki kusikia fact wame publish habari za kufungiwa. Hata ingekua kweli umefungiwa wamechelewa sanaaa coz mpaka panya wanajua tayari #TrueBoy keshakiwasha.”
Hata hivyo jana katibu mtendaji wa baraza hilo, Geofrey Mngereza, alihojiwa na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kudai kuwa wimbo huo haufai.
“Ni wimbo ambao haufai na ni msanii ambaye I dont know hata unashindwa kumpima ana akili ya namna gani, au kwa nini ameamua kufanya hivyo, lakini watu kama hao kwenye jamii wapo, ni kazi ambayo haifai katika jamii kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”, alisema.
“Anachofanya afikirie yeye ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii, kwa sababu mtu anayefanya namna hii asidhani kama anamdhalilisha mtu, anajidhalilisha yeye mwenyewe kwa sababu mtu yeyote ambaye anatoa lugha chafu, anafanya vitendo vya aibu, asidhani kama anamdhalilisha mtu, kwa hiyo yeye mwenyewe ni kama hayawani fulani tu”, aliongeza.
Kwenye wimbo huo Nay amewachana wasanii kibao wakiwemo Ommy Dimpoz, Wema Sepetu, Shetta na wengine.
0 comments:
Post a Comment