Shetta na Godfather wakutana tena kwa mradi mpya
Muimbaji wa ‘Shikorobo’, Shetta amekutana tena na muongozaji wa video wa nchini Afrika Kusini, Godfather kwaajili ya kile kinachoonekana wazi mipango ya kufanya video mpya.
Tayari muongozaji huyo amewahi kuongoza video mbili za Shetta ikiwemo ya Shikorobo aliyomshirikisha Kcee. Wawili hao wameshare picha kwenye akaunti zao za Instagram.
“Thanks Godfather for Having me In your office today, we shared A lot of things…! Let’s hope for the Best, Looking forward to do more business with u #Bless @i_am_godfather,” aliandika Shetta.
Naye Godfather ambaye jina lake halisi ni Mike ameandika: Initiating @shettatz into the Ogaranya circle…. Look out for his next level… This guy got something big coming. Stay tuned @shettatz.”
0 comments:
Post a Comment