Wachezaji wa DR Congo watuzwa magari ya kifahari baada ya kuchukua ubingwa wa Chan
Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa kila mmoja magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).
Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji gari gari la kifahari la thamani ya $60,000 (£40,000).
Wachezaji hao pia wamepewa nishani.
Chui hao walitwaa kombe kwa kuifunga Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.
Mwandishi wa BBC pia amesema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng’ambo kwa matibabu.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment