Young Killer: Nimeshawahi kuimba kabla ya kuanza kuchana
Rapper Young killer kutoka Mwanza amesema kuwa kabla ya kuwa MC alikuwa akiimba.
Young killer amekiri kuwa aliwahi kupata nafasi ya kurekodi kwa mara ya kwanza baada ya kusikika sauti yake ikiwa inafananishwa na msanii wa bongo fleva Keisha.
Ameyasema hayo kwenye mahojiano na kituo cha Radio City FM wakati akiwa anatambulisha wimbo wake mpya wa Insta Message.
“Mimi nilikuwa mwimbaji,nimeimba sana..kwa mfano Ali Kiba nilikuwa naimba album yake ya Cinderella yote,” alifunguka Young Killer
“Nakumbuka kuna producer alikuwa ananifurahia kwa sababu nilikuwa kachalii halafu kasauti kadogo,kanatoka kama Keisha anavyoimba..bhasi jamaa akanambia dogo nakupa ofa njoo urekodi.”
Source: City Fm
0 comments:
Post a Comment