Amitabh Bachchan na Ranaut washinda tuzo za Bollywood


Muigizaji mkongwe wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan na Kangana Ranaut wameshinda mataji makuu katika tuzo za kitaifa za filamu nchini India.



Bachchan alishinda tuzo ya muigizaji bora kwa jukumu lake katika Piku huku Ranaut akiwa muigizaji bora upande wa wanawake kwa filamu ya Tanu Weds Manu Returns.



Ranaut
Tuzo ya filamu bora lilichukuliwa na Bahubali huku Sanjay Leela Bhansali akijishindia mwelekezaji bora wa filamu ya Bajirao Mastani.

Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na serikali ya India.

Hiyo ni tuzo ya nne ya Bachchan.Alijishindia tuzo ya muigizaji bora mwaka 1990,2005 na 2009.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment