Sitamani kuwa kwenye uhusiano na mwanamke staa – Galaxy



Mwaka 2015 umekuwa wa neema kwa wasanii kibao wanaochipukia kwenye muziki wa Bongo Fleva.



Galaxy ni miongoni mwa wasanii wanaochipukia ambao wanafanya vizuri, ‘Tam Tam’ na ‘Mzuri Tu’ ni kati ya nyimbo zake zilizofanikiwa kufanya vizuri kwenye media mbalimbali mwaka 2015.

Akiongea na Bongo5, Galaxy amesema, ‘Sifikirii kuja kuingia kwenye mahusiano na staa’.

“Sifikirii kuja kuwa na mahusiano na staa yeyote wa kike. Kuwa kwenye uhusiano na staa wa kike huwa ni mazuri kibiashara, lakini ndani yake kuna changamoto nyingi ambazo unaweza ukajutia. Napenda niwe kama nilivyo sasa,” aliongeza Galaxy.

Baada ya kushindwa kuachia video ya ‘Mzuri Tu’ kwa sasa Galaxy amejipanga kuachia wimbo mpya pamoja na video yake mwishoni mwa mwezi wa nne.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment