Msanii wa Hip Hop kutoka Mwanza, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, amesema bado ana imani na msanii mwenzake Chid Benz na kuwataka watu wasimtenge.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumanne hii, Fid Q amesema kuwa Chid bado ana kipaji kikubwa.
“Ningependa kuwakumbusha watu Chid Benz bado ni msanii mkali, binafsi bado naweza nikamuindorse katika dili yoyote ya kuchana na akadeliver vizuri tu, mi nina imani naye na bado sijagive up on him kwa hiyo tusimu-underate eti kwa sababu saa hizi he is going through alot of difficult, bado yuko rehab na nini, talent ni talent jamaa ni talent na anayo, cha msingi tumsapoti na tumuombee tu asirudi kule alikojipeleka,” alisema Fid Q.
Hivi karibuni wasanii wengi wamejitokeza na kusema kuwa Chid Benz bado ana uwezo wa kurudi kwenye game, kwani bado wanamkubali kuwa ni msanii mkali.
0 comments:
Post a Comment