Label ya Diamond ‘WCB’ yafungua mlango kwa wasanii wa kike



Label ya Diamond Platnumz ‘WCB’ imetangaza neema kwa wasanii wa kike wenye vipaji.



Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, mmoja kati ya kiongozi wa label hiyo, Babu Tale amesema kama kuna msanii wa kike mwenye kipaji cha kumzidi Ruby wanamkaribisha.

“Tuna plan kuwapata wasanii wa kike lakini wenye vipaji vya ukweli, asikwambie mtu industry yetu ina wanawake wachache, tungepata wananwake wanne hata watano,” alisema Babu Tale

Pia Babu Tale alisema anatamani sana msanii Ruby angekuwa kwenye management yake, kwani ana uwezo mkubwa lakini kwa bahati mbaya tayari yuko chini ya management nyingine ya THT.

“Kwangu mimi ingekuwa Ruby hayuko chini ya THT, au hana management tungemchukua, lakini nasema hivi, kama anakuja mwanamke, awe na level ya kufanana na Ruby au kumshinda Ruby”, alisema Babu Tale

Pia Diamond aliweka wazi vigezo ambavyo msanii huyo wa kike avifikie ili aweze kuwa chini ya uongozi huo, pamoja na kujituma tofauti na walivyozoea kuwa hawawezi.

“Aweze kuandika mashairi, aandike nyimbo zake mwenyewe unajua kuna kitu kimoja, wanawake washajiwekea kuwa wao hawawezi, sio kweli hawataki kufocus na kujaribu”, alisema Diamond.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment