Manchester United wameanza kusoma alama za nyakati, mambo yanazidi kuwa magumu na wanaona kuna kila dalili wakampoteza David De Gea kwa Real Madrid.
Msimu uliopita Madrid walimkosa kumsajili De Gea kwenye dakika za mwisho, kipa huyo alionyesha kila dalili ya kuvutiwa kujiunga na mabingwa hao mara kumi wa uefa.
Hali inaonekana kuwa mbaya kwa United kwa sasa na kuna kila dalili wasishiriki michuano ya uefa msimu ujao kwa kuwa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa EPL. Mpaka sasa zimebaki mechi chache ligi hiyo kumalizika.
Na sasa United wanamfukuzia goli kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen, (23) ambaye anaonekana kushindwa kupata sana nafasi kwenye kikosi hicho.
Hata hivyo Liverpool nao wanamtaka Ter Stegen kuchukua nafasi ya Simon Mignolet ambaye ameonekana kutofanya vizuri msimu huu.
0 comments:
Post a Comment