Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amemlinganisha Marcus Rashford na Cristiano Ronaldo katika ufundi wa kupiga free kick.
Scholes amemfagilia Rashford kutokana na kiwango alichoonyesha na kusema kuna mengi yanakuja kutoka kwa mshambuliaji huyo kinda (pichani juu).
Rashford mwenye umri wa miaka 18, alijitambulisha kwa kishindo kwa mabao yake manne aliyofunga katika mechi zake mbili za kwanza akiwa na United msimu huu.
“Nimemuona akicheza tangu akiwa na miaka 14 au 15 na kisha katika kikosi cha Paul McGuinness (kikosi cha U-18 cha United),” alisema Scholes katika mtandao wa United We Stand.
0 comments:
Post a Comment